Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA-, ofisi kuu ya wafanyakazi ya Harakati ya Amal na kitengo cha kitaifa cha vyama vya wafanyakazi cha Hizbullah wamewaalika wafanyakazi, wazalishaji na wanavyama waaminifu wa Lebanon kushiriki kwenye mkusanyiko utakaofanyika katika uwanja wa Riyadh Al-Solh, Jumatano tarehe 27 Agosti 2025, saa kumi na moja na nusu jioni.
Mkusanyiko huu ni wa kulaani maamuzi mawili yaliyotolewa na serikali tarehe 5 na 7 Agosti 2025, ambayo yanapingana na maslahi ya juu ya taifa, Hati ya Makubaliano ya Kitaifa, na dhana ya kuishi kwa pamoja, pamoja na kuthibitisha haki ya Lebanon ya kulinda uhuru wake, na haki ya wananchi wake na muqawama (mapambano ya ukombozi) ya kutetea ardhi yao na kuikomboa kutoka kwa uvamizi wa "Israel".
Taarifa hiyo pia imesisitiza imani ya harakati hizo katika utakatifu wa muqawama na silaha zake halali, ambazo zinatumiwa kulinda taifa, na wito wa kulinda uamuzi wa serikali ya Lebanon dhidi ya shinikizo za nje, chini ya kaulimbiu:
"Haiwezekani tukubali udhalilishaji."
Imeongeza kusema:
"Enyi wafanyakazi na wazalishaji wa Lebanon, tumekuwa na subira kwa muda mrefu juu ya changamoto zinazoukumba taifa letu. Sasa umefika wakati wa kuonyesha msimamo wetu wa pamoja wa kitaifa."
Na ikaendelea:
"Tuna mkutano mkubwa wa kitaifa kuonyesha kupinga kwetu njia ya kunyenyekea na kujisalimisha, na kuunga mkono nguvu ya Lebanon na uhuru wake."
Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa:
"Msimamo huu ni uthibitisho wa haki yetu ya kulinda silaha zetu, ambazo zimeonyesha uwezo wa kuvunja nguvu za maadui, na ni haki yetu kupinga adui wa 'Israel' ambaye anavamia ardhi yetu, na kuikalia sehemu yake, na kuzuia uhuru wetu."
Imeongeza kuwa:
"Msimamo huu pia ni kwa heshima ya damu ya mashahidi wetu wapendwa, na kwa kuamini fundisho la Imam Musa al-Sadr kwamba 'Israel ni uovu mtupu na kushirikiana nayo ni haramu', na la Imam Khomeini kwamba 'Israel ni uvimbe wa saratani'."
Na imehitimisha kwa kusema:
"Enyi wafanyakazi na wazalishaji wa Lebanon, enyi wanavyama wapendwa, hebu iwe Jumatano tarehe 27 Agosti 2025 ni siku itakayokumbukwa katika historia ya harakati zenu, kupitia ushiriki wenu na sauti zenu zitakazosisitiza dhamira ya kusimama kidete na kukataa kunyenyekea. Msimamo huu ni uthibitisho wa nafasi ya muqawama na silaha zake halali katika kutetea heshima na uhuru wa taifa."
Your Comment